Uhusiano

Uhusiano

Kazi za kitengo

 1. Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja na Umma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.

      2.  Kuandaa machapisho mbalimbali ya Halmashauri.

   3.  Kupokea na kushughulikia malalamiko pamoja na kuratibu masuala ya kiitifaki ikiwemo kupokea wageni.

    4. Usimamizi Wa Mifumo Ya Kompyuta(System Administration) eneo hili linashughulikia usimamizi na uendeshaji wa mifumo yote ya kompyuta katika Halmashauri

5. Usimamizi Wa Mtandao Wa Kompyuta Pamoja Na Vifaa Vyake (Network And Hardware Adminstration).

6. Usimamizi Wa Benki Ya Takwimu(Database Administration)

7. Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails). 

 

JINSI MALALAMIKO YANAVYOTATULIWA.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeamua kuanzisha Ofisi ya MALALAMIKO ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa Serikali za Mitaa na Utawala bora.

 

Hivyo basi wewe mwananchi pamoja na Wadau wengine wote, mnajulishwa ili kuijua na kuitumia Ofisi hii kwa kutoa malalamiko juu ya KERO mbalimbali MAONI,USHAURI, MAPENDEKEZO au HOJA zinazojitokeza kutokana na utendaji wetu wa kazi za kila siku.

 

Kwa kufanya hivyo utaiwezesha Halmashauri yako kuboresha huduma mbalimbali zitolewazo kwa Wananchi wa Ilala.

 

Ili kuwasilisha Malalamiko, Maoni, Kero au Hoja mbalimbali unaweza kutumia njia mbalimbali za mawasiliano kama ifuatavyo:-

 

1. Kufika Ofisi ya MALALAMIKO iliyopo katika Ofisi za Manispaa ya Ilala – Jengo la Arnatoglou eneo la Mnazi Mmoja – Chumba Na. 02.

 

2. Kupiga simu kupitia namba ya simu 2180420.

 

3. Kutumia barua za kawaida kupitia anuani ya Posta:-

 

Mkurugenzi,

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,

S. L. P. 20950,

D’SALAAM.

 

 

Aidha majibu ya Malalamiko pamoja na hoja mbalimbali vitajibiwa kwa haraka kwa kupitia njia zifuatazo:-

 

1.Kujibu malalamiko kwa njia zifuatazo:

 

2.   Kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari:- Magazeti, Televisheni.

 

3.   Au njia nyingine yoyote ambayo itaonekana kufaa kulingana na uasili wa hoja au kero zitakazokuwa zimewasilishwa.

 

Je, Wajua kwamba:-

viii. Wewe ni kiungo muhimu sana ili kuboresha shughuli za utoaji huduma katika Halmashauri yako?

 

ix. Wewe ndio ‘Kioo’ cha Halmashauri unayetuwezesha kutambua maeneo tunayopaswa kuyafanyia marekebisho kwa haraka?

 

 

AI NA Y A M A L AL A M I K O

YANAYOPOKELEWAYALE YANAYOHUSU:

  1. Utoaji wa huduma – huduma za uzoaji taka mitaani.

 

  1. Malalamiko kuhusu maadili ya Mtumishi wa Halmashauri. Mf. Mtumishi kutumia madaraka yake kwa manufaa yake.

 

  1. Malalamiko kuhusu rushwa Mf. Mtumishi kupokea au kutoa chochote ili kupatiwa huduma.

 

  1. Malalamiko kuhusu uvunjaji wa haki za Binadamu.

 

PIA MALALAMIKO YANAWEZA KUPELEKWA OFISI RUFAA KAMA VILE:-

1.   Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa.

 

2.   Tume ya Maadili

 

3.   Tume ya Haki za Binadamu

 

4.   Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

 

5.   Kitengo cha Utawala B

 
JUU