Fedha na Biashara

Fedha na Biashara

Maombi yote mapya ya Leseni za Vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye fomu ya maombi, (Afisa Afya, Afisa Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata husika.

LESENI ZA VILEO:

Biashara ya Vileo inatekelezwa kwa kufuata Sheria ya Mwaka 1968, kifungu 28 (Liquor Licence Act No. 28 of 1968) na Marekebisho ya Sheria hiyo yaliyofanywa 2004.

UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA LESENI ZA VILEO:

Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yapitishwe na Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo Kata na yawasilishwe kwa Afisa Biashara anayeshughulikia Leseni za Vileo kwa utekelezaji.

Leseni za Vileo hutolewa kwa Vipindi viwili (2) ambapo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 01/04 hadi 31/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 01/19 hadi 31/03.

Maombi yote mapya ya Leseni za Vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye fomu ya maombi, (Afisa Afya, Afisa Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata husika.

ADA:

Maombi mapya na yanayorudiwa hulipiwa ada kama ifuatavyo:-

Tshs. 40,000/= kwa wale wanaonywesha pombe katika

maeneo yao ya Biashara (Retailers On).  Kwa kipindi kimoja.

· Wale ambao hawanyweshi pombe katika maeneo  yao (Retailers Off) wanalipia jumla ya Shs. 30,000/=.  kwa kipindi kimoja.

· Vilevile wanaouza au kufanya biashara ya Vileo kwa jumla (Wholesalers) wanalipia jumla ya Shs. 20,000/=.  Kwa kipindi kimoja.

· Pombe za kienyeji hulipiwa ada ya Shs. 12,000/= kila kipindi.

· Members club Shs. 60,000/= kwa kipindi.

Aidha wanaoendesha biashara ya Vileo bila kufuata  taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani kulipishwa faini pamoja na penalty au kufungiwa biashara zao.

KODI YA MAPATO

Kwa nini watu wanalipa Kodi?

Kodi ndicho chanzo pekee cha uhakika cha Serikali yoyote duniani cha mapato yake, ingawa katika falsafa ya kodi kuna sababu nyingine za kutoa kodi.

Mfano:-

-  Kulinda tabia za watu

- Kulinda viwanda

- Kupambana na mfumuko wa bei

- Kushawishi uwekezaji

- Kupunguza kipato kati ya mtu na mtu

- Kuhamisha utajiri wa sehemu moja kwenda nyingine n.k.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hupata mapato kutokana na vyanzo vikuu vine.

(i)    Mapato yake yenyewe

(ii) Ruzuku kutoka Serikali Kuu

(iii) Mikopo na

(iv) Misaada ya wahisani

Vyanzo vya Mapato katika Halmashauri ya Ilala ni:-

(i)    Faini ya kuvunja Sheria ndogo za Halmashauri

(ii) Kodi ya nyumba za Halmashauri zilizokuwa za shirika la nyumba (NHC).

(iii) Kodi ya Huduma za Jiji (City Service Levy).

(iv) Fedha za vyanzo vya kodi vinavyokusanywa na Jiji (Tanzania Parking System, faini za mahakama ya Jiji na Asilimia ishirini (20%) kutoka Sumatra).

(v) Ada ya usafiri na maegesho ya Taksi.

(vi) Leseni ya pombe za kigeni

(vii)   Kodi ya nyumba za kulala Wageni.

(viii) Ushuru wa Masoko na vizimba

(ix) Ushuru wa matangazo na kuzingira (uzio unaozungushiwa mabati).

(x) Ada ya uchunguzi wa Ramani

(xi) Ada ya Minara ya Mawasiliano

(xii)   Kodi ya Majengo

(xiii) Leseni za Uvuvi

(xiv) Ada ya kuchanga na uchangiaji wa Hospitali.

(xv)   Ada ya machinjio na ukaguzi wa nyama.

(xvi) Kodi ya nyumba za Starehe na Viwanja vya Michezo.

I.  CITY SERVICE LEVY

Kodi hii ni matokeo ya Sheria ya fedha namba 9 ya 1982 kifungu cha 6 (1)(U).

Kodi hii hulipwa na makampuni, taasisi na biashara mbalimbali zilizosajiliwa VAT.  Kutokana na mauzo ghafi kwa kiwango kisichozidi asilimia 0.3.

Kwa kawaida kodi hii hukusanywa mara nne kwa mwaka kila baada ya miezi mitatu na utaratibu wa malipo ni kama ifuatavyo:-

· Mlipakodi Atatakiwa awasilishe hesabu ya mauzo yake katika Ofisi za Halmashauri, ambapo atawakabidhi wataalamu wa kutoza kodi hiyo ambao baada ya kuzidisha na hiyo asilimia 0.3 atalipa kiasi kinachopatikana.

Mfano mfanyabiashara ameuza kiasi cha Shs. Milioni moja kwa miezi mitatu, i.e. 1,000,000/= itazidishwa na asilimia 0.3 ambazo ni:- 1,000,000 x 0.3 kiasi kinachopatikana yaani Shs. 3,000/= ndizo anazopaswa kulipa, na katika ulipaji, mlipa kodi anajaza fomu maalumu ambazo zinapatikana katika Ofisi za Halmashauri na kuambatanisha na mauzo yake na baada ya kufanya malipo anapewa risiti ambayo anapaswa kuiweka tika kumbukumbu zake kwa ajili ya ukaguzi n.k.

Aina ya Makosa yatakayosababisha kutozwa faini/adhabu:-

· Mtu yoyote anayetakiwa kulipa kodi akishindwa kuwasilisha hesabu zake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ndogo na inapobainika kuwa amefanya makundi.

· Kodi ambayo haijalipwa kwa wakati kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ndogo itatozwa na riba ya  faini ya asilimia kumi na tano (15%) kwa mwezi na zitatakiwa kulipwa pamoja na kodi inayodaiwa.

· Mtu yoyote ambaye bila sababu za msingi atashindwa:-

(a) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa.

(b) Kutunza kumbukumbu, kitabu au hesabu.

(c) Kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi.

Mtu yeyote bila sababu za msingi:-

(a) Akifanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwa sahihi.

(b) Akitoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa kodi.

(c) Akiandaa au kutengenezewa vitabu vya uongo vya Mahesabu au kumbukumbu.

(d) Atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Muidhiniwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ndogo atakuwa anatenda kosa.

Mtu yeyote atakayevunja masharti ya Sheria ndogo hizi atakuwa anatenda kosa na atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) au kifungo cha miezi isiyozidi (12) kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja.

NB:  Pamoja na adhabu atakayotozwa mkosaji kwenye kif. Na. 17 (1). Pia atawajibika kulipa gharama nyingine za Halmashauri.

MABANGO

Ushuru wa mabango hutozwa kutoka kwenye tangazo au maandishi yanayoashiria utangazaji wa kibiashara.  Utozaji wa kodi ya mabango husimamiwa kwa kutumia sheria ndogo iliyokuwa ya tume ya Jiji kwa viwango vya Tshs. 6,000/= kwa futi moja kwa mwaka, kwa bango ambalo haliwaki taa na Tshs. 8,000/= kwa futi kwa bango linalowaka taa.

Utaratibu wa Malipo:

Malipo ya Matangazo hulipwa kwa kipindi cha kuanzia 30 June Julai 01 hadi mwaka unaofuata.

· Mfanyabiashara anaweza kulipa malipo hayo kwa mwaka mzima au kwa awamu nne tofauti zinazofanana (equal Instalment.)

· Mfanyabiashara atakayetaka kulipia kodi hii ya Matangazo kwa mara ya kwanza muda wowote baada ya Julai atapigiwa hesabu zake kuanzia muda alioanza malipo hadi mwisho wa mwaka wa fedha badala ya kulipa malipo ya mwaka mzima.

Malipo ya Adhabu:  kwa mujibu wa kifungu namba 79 (2,3,4).

Utaratibu.

Mfanyabiashara atapewa notisi ya siku (14) kumi na nne baada ya siku alizotakiwa kulipia, na kufuatiliwa ili alipe kodi kufikia tarehe 31 Machi ya mwaka husika.

· Matangazo ya Ushuru yasiyolipiwa hadi kufikia tarehe 31 Machi, baada ya kupata notisi, Mfanyabiashara atatakiwa kulipa deni husika na malimbikizo pamoja na asilimia 10% (compound interest) ambayo itachajiwa kwa kila mwezi na kwa kila sehemu ya kiwango ambacho hakijalipwa.

· Endapo kodi ya Matangazo haitalipwa hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha ukiairishwa kwenye Sheria ndogo ya Halmashauri.  Mfanyabiashara atatozwa Deni la kodi aliyotakiwa kulipa na riba pamoja na 30% ya riba kwa kila mwezi.

TARATIBU ZA KUSAJILI TAKSI:

Magari madogo yanayoshughulika na biasharaTaksi/Tours na Private Hires husajiliwa na kitengo cha Biashara Manispaa ya Ilala na kupewa namba za usajili chini ya Sheria ndogo ya mwaka 1968.

Sifa za Takisi

Taksi

1. Uzito usiozidi ¾ ya tani.

2. Rangi Nyeupe

3. Milango mine kwa magari yote “RHD” na “LHD”.

4. “Plate” namba nyeupe.

5. “Neon Lamp” inayofanya kazi.

6. Abiria wasiozidi watano pamoja na Dereva.

Carrier:  ni hiari ya mwenye gari kuweka au kuacha mstari wa kijani na baka la njano sifa hii imeondolewa haipo tena.

Tours/Private Hire:

 1. Rangi ni yoyote.
 2. Milango mine kwa magari madogo
 3. Milango mitatu kwa mabasi madogo
 4. Yasiyozidi abiria 16 -20
 5. Nembo ya Kampuni ubavuni

 1. Kibali cha Eneo la Maegesho ya magari hayo Eg. Hoteli za Kitalii
 2. Business Licence Tax Clearance Certificate (TRA).
 3. Kadi ya Gari Original.
 4. Stikker (TRA).
 5. Licence of Taxi Cab (Income Tax Department)
 6. Vehicle inspection Report (Trafic Police).

Leseni ya Biashara ya (Car Hire/Tour Operator) toka Wizara ya Viwanda na Biashara.

 1. Leseni ya kuendesha Biashara ya Uwakala wa utalii – T.A.L. toka Wizara ya mali asili na Utalii.

 1. Rangi: Magari madogo (Car Hire/Private Hire) yanayoendesha Biashara za kuendesha watalii yanaruhusiwa kuwa na Rangi ya Aina yeyote.

Magari yanayosajiliwa yanapaswa kutimiza Taratibu/Masharti yafuatayo:-

A:  Viambatanisho vya usajili wa Magari Madogo ya Abiria (Taxi Cabs) mwaka 2008.

 1. Kila Mfanyabiashara wa Taksi lazima awe na Kituo cha kuegesha Gari lake kilichosajiliwa na Manispaa husika.

 1. Kadi ya Gari (Original

· Rangi ya Gari iwe nyeupe

 1. Business Licence Tax clearance certificate toka – (TRA)

 1. Sticker ya Mapato toka – (TRA)

 1. Licence of Taxi Cab – Toka TRA.

 1. Vehicle Inspection report (Traffic Police).

B: Gharama za usajili Taksi zinazoegeshwa kwenye maeneo rasmi ya Manispaa.

1. Usajili wa gari   -  Shs. 20,000/= kwa mwaka

2. Maegesho -  Shs. 36,000/= kwa mwaka

3. Ada ya Kituo Shs.  5,000/= kwa mwaka.

Jumla Tshs. 61,000/=

MAGARI YANAYOEGESHWA KWENYE KITUO CHA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT

1. Watalipia kibali cha maegesho ya maeneo hayo Ada ya usajili Shs. 20,000/= kwa mwaka.

· Magari yatakayosajiliwa kupitia Kampuni ya Tours/Private Hire, yanaambatanisha vibali na kulipa ada ya usajili ya sh. 20,000/= tu kwa mwaka.

· Vituo vya Taksi

Vituo vyote vya Taksi ni mali ya Manispaa.

i.   Ada ya kituo hulipwa na madereva wanaotumia kituo hicho, ambayo ni Shs. 5,000/= kwa kila gari/Dereva kwa mwaka.

Upatikanaji wa Kituo: Waombaji wanapaswa kutuma maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa husika kupitia kwa Kamati za Maendeleo za Kata; Mhandisi wa Manispaa hukagua na kutoa maamuzi na waombaji hujibiwa kama panafaa ua hapafai.

Kama panafaa waombaji wanatakiwa kulipia malipo ya Kituo kwa Mhandisi wa Manispaa hutoa namba ya kituo.

USHURU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI (HOTEL LEVY)

· Ushuru huu unalipwa kwa kufuata Sheria ya nyumba za kulala Wageni (The Hotels Act) ya mwaka 1965 sura ya 105 kifungu cha 26 (2) pamoja na  Marekebisho yake ya mwaka 2002 (The Hotel Act Wap. 105) toleo la mwaka 2002.

· Asilimia 20% ya jumla ya Mapato yanayotokana na malipo ya wateja wanaolala kwenye nyumba husika ya wageni hutozwa ushuru kwa kila mwezi.

· Mlipaji wa ushuru huo ni mmiliki wa Biashara ya nyumba hiyo ya kulala wageni.  Malipo hayo kufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 ya kila mwezi.

Taratibu za Ushuru wa Nyumba za kulala wageni ni kama ifuatavyo:-

· Mfanyabiashara wa nyumba ya kulala Wageni anapaswa kujaza Kitabu cha Wageni wanaolala au kuingia kwenye nyumba hiyo kila siku (visitors book).

· Mwendesha Biashara ya nyumba ya kulala wageni anatakiwa ajaze fomu za wageni wanaopangisha hapo kila siku (Daily occupancy Return) na za kila mwezi (Monthly occumpancy Return).

· Ushuru huu hulipwa na Wafanyabiashara wa Nyumba za kulala wageni ambao hawajasajiliwa kulipa VAT.

Adhabu:

· Asilimia 25% ya Ushuru wa Hoteli.  Itatozwa endapo mlipaji atakuwa amechelewa kulipia zaidi ya siku saba kifungu cha 32(a).

· Ongezeko la asilimia 10% itakayokuwa inaongezeka kwa kiwango cha Ada ambayo haijalipiwa kwa kila siku thelathini (kifungu cha 32 (b) kinaelekeza.

· Kukiuka taratibu za ulipaji wa Hoel levy faini ni Sh. 500,000/= (laki tano).  Mfano kudanganya mapato, kutokuwa na kitabu cha kumbukumbu nk.

· Kukiuka ulipaji wa Hotel Levy faini ni Shs. 2,000,000/= Mfano; Nyumba ya Wageni ambao haijalipa Hotel Levy tangu kuanzishwa kwake.

LESENI ZA BIASHARA

UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA:

Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake  yaliyofanyika Juni 2004.  Mwombaji wa leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN 211 (Business licence application form).

Leseni za Biashara zimegawanyika katika makundi mawili:-

KUNDI A:  Leseni hizi hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mfano:

· Uagizaji bidhaa toka nje (import licence).

· Kusafirisha bidhaa nje (Export licence).

· Wakala wa Mali (Estate Agent).

· Hotel za Kitalii (Tourist Hotel & Lodging).

· Wakala wa kupokea na Usafirishaji mizigo. (Clearing and Forwarding/Freight Forwarders) n.k.

KUNDI B:  Hizi hutolewa na Halmashauri za Manispaa husika.

Mfano:

· Wakala wa Bima (Insurance Agent).

· Vipuri (Spare Parts, Machine tools).

· Maduka ya dawa za Binadamu/Mifugo

· Viwanda vidogo (Small Scale Manufacturely and selling).

· Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale and Retail trade) n.k.

MASHARTI YA KUOMBA NA KUPEWA LESENI ZA BIASHARA:

 • Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara (Certificate of Registration or Incorporation).

 • Kama ni Kampuni mwombaji awe na memorandum and: Articles of Association” ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.

Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi.

 • Awe na mahali/Eneo linalokubalika kwa aina  ya biashara anayoiomba na isiwe vibanda vilivyopo kando kando ya barabara.

 • Awe na TIN Certificate.

 • Awe na hati ya kuthibtisha uraia wake e.g. photo copy ya passport ya Tanzania, cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo (Affidavit).  Kama ni mgeni awe na hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Resident Permit Class “A”.

 • Masharti mengine ya kupata leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha, eg. Mgahawa inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.

 • Hati ya utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalam.

 • Maombi mapya yatapitia ngazi za  Mipango Miji, Biashara, Afya na kisha kikao cha Kamati ndogo ya leseni.

MALIPO: Kutokana na marekebisho ya sheria ada za leseni hulipwa kulingana na mapato ya mfanyabiashara.  Kwa wale ambao mapato yao hayafiki Mil. 20 wanapata leseni bila ya kulipia ada yeyote.  Wale wenye mapato  zaidi  ya hapo hulipa shs.  20,000.-.  Hata hivyo leseni mpya zote zinapatikana bila kulipiwa ada.

Leseni za biashara hazijafutwa.

Kuna mabadiliko yafuatayo:-

· Hakuna Ada ya leseni itakayolipwa na waombaji wote wapya kuanzia mwaka 2004 na kuendelea.

· Umri wa leseni ni kwa Maisha yote (Life – spare of business licence).  Kwa mujibu wa sheria ya leseni za biashara kifungu Na.21 na 24

Adhabu:  Mfanyabiashara atakayekutwa anafanya biashara bila kuwa na leseni atatozwa faini ya kuanzia shs. 50,000/- hadi 100,000/- au apelekwe Mahakamani hii imeainishwa kutoka kifungu Na. 10(1) (b).

 

N.B:  Sheria ya utoaji wa leseni za biashara inaendelea kufanyiwa Marekebisho na Mfumo mzima wa utoaji wa leseni utabadilika.  Punde mabadiliko hayo yakikamilika wafayabiashara watajulishwa 

JUU