Leseni, Vibali, Kodi, Fomu za sajili

Leseni, Vibali, Kodi, Fomu za sajili

SHERIA NA TARATIBU ZA KUPATA  HUDUMA ZA LESENI MANISPAA YA ILALA

 

S / n

 

SHERIA / KANUNI

 

UTARATIBU WA KUFUATWA

 

MUHUSIKA

 

MWASILIANO

 

1

Sheria ya leseni za biashara Na 25 ya 1972

Kujaza fomu ya maombi (Fomu Na tfn21) na kuambatanisha nyaraka zifuatazo

- Kwa jina la biashara aweke nakala ya hati ya kuandikisha jina la biashara au kampuni kutoka BRELA

- Hati ya uthibitisho wa uraia  (Anaweza kuweka cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo cha Mahakama)

- Uthibitisho wa kuwa na mahali [pa kufanyia biashara( Hati ya nyumba au mkataba wa pango au stakabadhi ya malipo ya kodi ya majengo)

- Hati ya kusajiliwa kama Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA)

- Kwa waombaji ambao sio raia wa Tanzania wawe na hati ya kuishi nchini ya daraja ‘A’ na kwa wawakilishi wa mfanyabishara au kampuni iliyoko nje ya nchi wawe na hati ya Kiwakili ( Power of Attorney)

- Kwa biashara za kitaalamu awe na cheti cha utalaamu

- Kwa biashara zinazodhibitiwa na Mamlaka za udhibiti awe na hati kutoka Mamlaka husika.

Kwa waombaji wanao huisha leseni zao watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita.

Denis Mrema

Afisa Biashra wa Manispaa

0715295628

2

Sheria ya leseni za vileo Na 28 ya 1968 na marekebishao yake ya 2012

Muombaji atajaza fomu ya maombi

- Atatakiwa kuambataisha Hati ya Mlipa kodi-TIN kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

-  Kwa waombaji wapya fomu ipitishwe kwa;

a) Kwa Afisa Afya wa kata

b) Afisa Mipango miji

c) Kituo cha Polisi kilicho jirani

d)   Mwenyekiti kamati ya maendeleo ya kata

e) Afisa Biashara

f) Mwenyekiti Bodi ya vileo.

- Kwa waombaji wanaohuisha leseni  watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita na kupitisha fomu yake kwa Mwenyekiti kamati ya Maendeleo ya Kata.

NB: Mabadiliko huweza kutokea kutokana na maamuzi ya kikao cha Bodi.

 

Monica M. Mbombwe

Afisa Biashara

0717943415

3

Hotel levy Act ya 1973

Kodi hii hulipwa mara moja kabla ya tarehe 7 ya kila mwaezi. Mlipaji anatakiwa kuja na kitabu cha wageni, Afisa Biashara husika hukokotoa kiasi cha kodi kutoka katika kitabu cha wageni. Kiasi cha kodi ni asilimia ishirini ya mapato ya mwezi 

 

 

Athumani Mbelwa

Afisa Biashara Mkuu II

0754269451

4

TFDA Sheria No. 8 kifungu No. 18 (2)

Utaratibu:

Kujaza form No. TFDA 0001. Kwaajili ya usajili wa jengo. Pia kujaza form No. TFDA0003 kwaajili ya leseni.

Kisha mwombaji atawasilisha fomu hizo kwa Afisa Afya wa kata husika kwaajili ya ukaguzi na kuendelea na taratibu za malipo.

 

 

Ally Babu

Afisa Afya Mkuu

0713065586

5

Mabango: sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa sura ya 288 kifungu Na. 89 (1)

kujaza fomu ya maombi na kuiwasilisha kwenye ofisi ya mapato kisha Afisa husika kwenda eneo husika kwa ukaguzi ili kubaini ukubwa na aina ya bango aidha kujiridhisha kama eneo linafaa kwa shughuli hiyo.

Christina Changwala

 

0713598668

5

Kodi ya huduma ya Jiji; sheria ya Fedha ya Serikali za mitaa sura ya 290 kifungu Na. 6 (01) na 16 (1)

Kujaza fomu Na. ….. na kuiwasilisha kwa Afisa husika kwaajili ya ukokotoaji wa kiasi cha kodi inayopaswa kulipwa. Tozo ni asilimia 0.3 ya mapato ya kipindi husika.

Witty Kafanabo

0717153306

6

Sheria ya afya ya jamii ya 2009 sehemu ya Sehemu ya 27.

Majengo ya bisahara yanapaswa kukaguliwa, Afisa Afya  ana uwezo kwa mujibu wa sheria Kufanya Ukaguzi wa kiafya kwenye jengo la biashara, na kujiridhisha na hali ya kiafya ya jengo.

 

Utaratibu:

Waombaji wa leseni za  Hoteli za kawaida, Vilabu vya pombe. Watengenezaji na wauzaji wa vyakula na Vinywaji. Majengo wanamo fanyia shughuli hizo yanapaswa kukaguliwa na Afisa Afya:

Mwombaji aende kwenye ofisi ya kata husika na aonane na Afisa Afya wa Kata kwaajili ya ukaguzi, kisha kuandaa taarifa ya ukaguzi na kuiwasilisha kwa Afisa Afya Mkuu wa Manispaa, pamoja na maombi ya leseni.

 

Afisa afya

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

0715841197

7

Sheria ya afya ya jamii ya 2009 sehemu ya 150 (6)

 

Mhudumu / mtumishi yeyote katika nyumba za kulala wageni, hotel au sehemu yoyote inayo tolewa huduma ya vinywaji au vyakula. Anapaswa kupima afya kwa mujibu wa sheria hii.

 

Utaratibu:

Huduma ya kupima afya kwa Manispaa ya Ilala inatolewa katika vituo vya tiba vifuatavyo:-

a. Hosipitali ya Amana

b. Kituo cha Afya Buguruni

c. Hospitali ya Mnazimmoja

 

Afisa afya

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

0715841197

8

Sheria ya mamlaka ya miji namba 2 ya mwaka 1983. na sheria ndogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya viwango vya kodi ya majengo ya mwaka 2003.

 

Wathamini hufanya uthamini wa jengo kisha mwenye jengo hupaswa kufuata hati ya madai, akipokea hati hiyo mwenye jengo hutakiwa kulipa kodi husika ndani ya siku 30 toka alipopokea hati hiyo.

Viwango vya kodi vimegawanyika katika makundi mawili;

d. Nyumba za makazi hutozwa 0.15% ya thamani ya jengo sambamba na ukubwa wa eneo.

e. Nyumba za biashara hutozwa 0.2% ya thamani ya jengo sambamba na ukubwa wa eneo.

 

Stelah Mgumia

0713521916

9

Sheria ya leseni za Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.

 

Kila anayejihusisha na shughuli za uvuvi na uuzaji wa samaki anapaswa kuwa na leseni ya uvuvi kwa mujibu wa sheria hii.

Utaratibu:

Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi ya leseni namba 3C inayo dodosa jina na anuani ya mwombaji, kisha kuambatanisha Picha tatu za saizi ndogo yaani passport size.

Ada ya leseni ya Uvuvi ni dola 10 za Kimarekani inalipwa kwa shilingi ya Kitanzania kwa kulinganisha na bei ya kuvunjia ya siku husika

Msongo Songolo

Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

 

0712539738

 

 

 

 

 

 


 

   

JUU