DC-MJEMA AWAONGOZA WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA KUFANYA MAZOEZI

DC-MJEMA AWAONGOZA WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA KUFANYA MAZOEZI

Jumamosi ya tarehe 11 Februari, 2017 ilikuwa ni siku ya uzinduzi wa kampeni ya kufanya mazoezi kwa Wilaya ya Ilala, ambapo Watumishi wa Manispaa ya Ilala, timu ya Mkoa wa Dar-es-Salaam wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, waliungana na Wananchi toka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala kwa kufanya mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu waRais linaowataka Watumishi wa Halmashauri kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwezi.


Uzinduzi wa kampeni hiyo uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema na uliambatana na kaulimbiu: "Afya ni mtaji wa Maendeleo. Nitailinda kwa gharama nafuu kwa kufanya mazoezi.".


Aidha, uzinduzi huo wa mazoezi uliambatana na makabidhiano ya Katiba ya Michezo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema alimkabidhi katiba ya michezo Mkurugenzi wa Mnispaa hiyo Ndugu Msongela Palela, halikadhalika Mkuu wa Wilaya alikabidhi na Katiba ya Vikundi vya Mbio fupi 'Jogging' kwa Katibu wa Mbio fupi Wilaya ya Ilala, ambapo sasa itawalazimu kusajili Vikundi vyote vya Mbio fupi.


Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndungu Msongela Palela ameeleza kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kwa Watumishi kila siku ya Ijumaa ili kujikinga na magonjwa yasioyaambuza kama vile Kisukari na Presha. 

Uzinduzi wa Kampeni ya Mazoezi Wilaya ya Ilala

JUU