Idara ya Mipango,Takwimu na Ufatiliaji

Idara ya Mipango,Takwimu na Ufatiliaji

IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI

Idara ya  Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika,  usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji.  Idara hii inaongozwa na Mchumi wa Manispaa na imegawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:-

Ø  Mipango na Sera

Ø  Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo

Ø  Uwekezaji

Ø  Tafiti na Takwimu.

Ø  Sehemu ya TASAF

  Sehemu ya Mipango na Sera.

Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-

Ø  Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.

Ø  Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.

Ø  Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD.

Ø  Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.

Ø  Kusimamia uandaaji wa mipango kazi (Action Plans) ya bajeti za kila mwaka na kuziwasilisha katika ngazi husika..

Ø  Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ø  Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)

Ø  Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri

Ø  Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali

Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi ya

maendeleo.

Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-

Ø  Kuratibu uandaaji wa taarifa za Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya  2015 - 2020

Ø  Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

Ø  Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani

Ø  Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya muda mrefu, kati  na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo

Ø  Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.

Ø  Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Manispaa kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.

Ø  Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka

Ø  Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.

Ø  Kuandaa taarifa za matukio ya kila wiki na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.

Sehemu ya  Uwekezaji.

Sehemu hii hushughulikia mipango ya uwekezaji katika Halmashauri ya Manispaa kwa kufanya yafuatayo:-

1. Kuratibu na kusimamia maandalizi ya mipango ya uwekezaji ya Halmashauri.

2. Kuratibu utekelezaji na uandaaji wa taarifa za mipango ya uwekezaji

3. Kuratibu utekelezaji wa miradi ya DMDP

Sehemu ya  Utafiti na Takwimu.

Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-

Ø  Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri ikihusisha takwimu za LGMD.

Ø   Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.

Ø  Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa

Ø  kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.

Ø  Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2012/13 – 2016/17

Ø  Kuratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Ø  Kuandaa taarifa za utatuzi wa kero na malalamiko kila wiki na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa

Sehemu ya TASAF

Utekelezaji wa shughuli za awamu ya tatu ya TASAF Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III PSSN) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala uliendelea kama kawaida ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2016 malipo kwa kaya maskini 6,262 kutoka katika mitaa 74 iliyopo kwenye mpango yalifanyika.

Vile vile Halmashauri imetoa mafunzo kwa wataalamu wa Elimu msingi, Elimu sekondari pamoja na Afya sambamba na kuendelea na zoezi la usambazaji wa fomu za kutimiza masharti ya elimu na afya kwa kuziwasilisha katika shule na zahanati za mitaa husika pamoja na kukusanya zile zilizosambazwa katika kipindi cha Novemba/Desemba.Vilevile madaftari pamoja na fomu za masharti ya elimu kwa shule zilizopo nje ya Halmashauri zimepangwa kulingana na wilaya/mkoa unaohusika na zimewasilishwa kwa mratibu wa mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji.

Katika kipindi cha utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2016 Halmashauri imeendelea na  utekelezaji wa zoezi la malipo ya Kaya Maskini ambapo shughuli zilizofanyika ni pamoja na malipo ya kaya maskini ya awamu ya tatu na awamu ya nne yaani malipo ya  mwezi Januari na Februari, 2016 (January/February Window Period) pamoja na malipo ya  mwezi Machi na Aprili, 2016 (Machi/Aprili Window Period). Katika kipindi cha malipo cha mwezi  Januari na Februari Halmashauri ilipokea kutoka TASAF  jumla ya sh. 301,243,500.00  ambapo kati ya fedha hizo fedha zilizokwenda katika ngazi ya jamii  kwa ajili ya malipo ya kaya maskini na asilimia ya mtaa ni sh. 272,336,295.45  na  sh. 28,907,204.55  zilizobaki katika ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya uwezeshaji wa usimamizi na ufuatiliaji wa zoezi la malipo.  Vilevile katika kuongeza ufanisi wa ujazaji wa Fomu za Kutimiza mashrti ya Elimu na Afya Halmashauri imefanya mafunzo kwa wataalam mbalimbali wa ngazi ya kata wanaosaidia zoezi la malipo katika ngazi ya jamii na jumla ya wataalam 188 Walipatiwa mafunzo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Kati yao 110 ni waalimu wa shule za msingi, 51 ni walimu wa shule za sekondari na pia  wataalam wa Afya 27 wamepatiwa mafunzo. Katika kipindi cha malipo cha mwezi  Machi na Aprili Halmashauri ilipokea kutoka TASAF  jumla ya sh. 298,782,000.00  ambapo kati ya fedha hizo fedha zilizokwenda katika ngazi ya jamii  kwa ajili ya malipo ya kaya maskini na asilimia ya mtaa ni sh. 270,000,000.00  na  sh. 28,671,000.00  zilizobaki katika ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya uwezeshaji wa usimamizi na ufuatiliaji wa zoezi la malipo. Aidha katika kuhakikisha Halmashauri inakuwa na taarifa sahihi za watoto wanaotakiwa  kutimiza mashrti ya Elimu na Afya waalimu na wataalam wa afya wa ngazi ya kata walishiriki zoezi la malipo kwa kuandikisha watoto kutoka katika familia za walengwa wa mpango ambapo jumla ya wataalam 101(waalimu 74  na watumishi wa afya 27) walishiriki zoezi hilo katika mitaa 74 iliyoko kwenye mpango. 

JUU