Idara ya Afya

Idara ya Afya

IDARA YA AFYA

 

HUDUMA ZA AFYA

Idara inawajibika na kutoa huduma za afya katika hospitali,vituo vya afya na Zahanati, Kwa sasa idadi ya vituo vinavyotoa huduma kama ifuatavyo:-

HOSPITALI ZA SERIKALI

HOSPITALI BINAFSI NA MASHIRIKA

IDADI

Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili, Ocean Road, Moi

1

0

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa/Wilaya

1

0

Hospitali

1

7

7

Vituo vya Afya

3

21

21

Zahanati

24

119

119

 

  HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inayo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa 1 ambayo ni Hospitali ya Amana. Hospitali hii ipo maeneo ya Ilala ambapo inatoa huduma kwa wagonjwa waliopewa rufaa kwenda mahali hapo kutoka vituo vyote vya ndani ya Manispaa. Hospitali hii pia  inapokea wagonjwa wa msamaha, Bima na uchangiaji na ina jumla ya vitanda 360.  Huduma zinazopatikana hapa ni pamoja na huduma za:-

· Maabara

· Upatikanaji wa dawa kupitia pharmacy

· Vipimo vya x-ray

· Upasuaji (Theatre)

· Mazoezi ya viungo (Physiotherapy)

· Chumba maalum cha kuhifadhi maiti (Mortuary)

· Clinics mbalimbali zikiwemo

· Tiba kwa wagonjwa wanaoishi na VVU

· Mama na mtoto

· Kisukari

· Ushauri nasaha na kupima

· Magonjwa ya kina mama

· Magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana

· Moyo na shinikizo la damu


HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

Hospitali ya Mnazi Mmoja ipo katika Kata ya Mchafukoge Manispaa ya Ilala ndani ya jiji la Dar es salaam. Historia ya Hospitali hii ni kwamba kuanzia mwaka 1950 hadi mwaka 1989 ilikuwa katika kiwango cha zahanati, mwaka 1990 ilipanda hadhi na kuwa kituo cha Afya, mwaka 2012 ilitangazwa kuwa hospitali kutokana na huduma kutoka na kuwepo kwa huduma zinazopatikana Hospitali.

Kutokana na kuwa iko katikati ya Jiji la Dar es salaam usafiri ni rahisi kwa watu binafsi hata jamii (Public Transport). Hospitali hii inahudumia wagonjwa toka sehemu mbalimbali za Dar es salaam hata mikoa ya karibu mfano Morogoro, Pwani na Tanga. Hospitali ina watumishi wapatao 260 wa kada mbalimbali wanaotoa huduma masaa 24 kwa wagonjwa wa nje na wa ndani na hasa huduma za mama na mtoto. Idadi ya wagonjwa wanaopata huduma kati ya 800 – 1000 kwa siku.

Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

· Upasuaji Mdogo (minor theatre) na pasuaji wa kinamama wajawazito na watoto wachanga

· Kliniki ya Kifua kikuu/Ukoma TB/HIV

· Kiliniki ya kisukari na shinikizo la damu

· Ushauri nasaha (VTC)

· Kliniki ya wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (CTC)

· Kitengo cha macho

· Kitengo cha meno

· Kitengo cha maabara

· Kitengo cha madawa (Pharmacy)

· Ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya UKIMWI (PITC)

· Unyanyasaji wa kijinsia (GBV)

VITUO VYA AFYA

KITUO CHA AFYA CHANIKA

 

Kituo cha Afya Chanika kipo nje kidogo ya Dar es salaam Kata ya Chanika Tarafa ya Ukonga ni umbali wa Km 32 kutoka Amana.  Chanika ina jumla ya wakazi 43,912 (Census report 2013) na ina mitaa 8. Kituo hiki kinatoa huduma kwa wakazi wa Gongo la Mboto, Majohe, Buguruni, Zingiziwa, Msongola, Pugu, Homboza, Kitanga, Msimbu na Masaki.

Huduma zinazopatikana

Huduma kwa wagonjwa wa nje zinatolewa masaa 24. Aidha huduma za Wazazi, maabara, ushauri nasaha, tiba kwa wagonjwa wa Kifua kikuu na ukoma,  huduma ya mama na mtoto, chanjo, huduma za jamii  na majumbani, vijana, huduma ya kinywa na meno, huduma ya dawa kwa waviu pia hutolewa.  Kituo kina jumla ya watumishi 54. Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kina mama na watoto kupitia ufadhili wa Jamhuri ya Watu wa Korea Kusini unaendelea gharama ya mradi huu ni takribani Tshs. 8.8 bilioni, ujenzi huu unatarajia kukamilika Desemba, 2016.

KITUO CHA AFYA BUGURUNI

Kituo cha Afya Buguruni kipo eneo la Buguruni kwa Mwini Amani Kata ya Buguruni kwa jina lingine wakazi wamezoea kuita kituo cha plani. Kito hiki kimepakana na Kata ya Vingunguti na barabara kuu ya Mandela.

Huduma zinazopatikana

Huduma kwa wagonjwa wa nje ni masaa 24.  Huduma za wazazi, maabara, ushauri nasaha, tiba kwa wagonjwa wa Kifua kikuu na ukoma.  Huduma ya mama na mtoto, chanjo, huduma za jamii na za majumbani, vijana, huduma ya kinywa na meno, huduma ya dawa kwa waviu, Utrasound, upasuaji mdogo pia hutolewa katika kituo hiki

3.  KITUO CHA AFYA PUGU

Kituo cha Afya Pugu kipo pembezoni mwa barabara iendayo Chanika imepakana na Shule ya Sekondari Pugu Kajiungeni.

Huduma zinazopatikana

Huduma kwa wagonjwa wa nje ni masaa 24. Huduma za Wazazi, maabara, ushauri nasaha tiba kwa wagonjwa wa Kifua kikuu na ukoma.  Huduma ya mama na mtoto, chanjo, huduma za jamii majumbani, vijana, huduma ya kinywa na meno, huduma ya dawa kwa waviu, upasuaji mdogo, wodi ya kulaza wagonjwa.

ZAHANATI ZA SERIKALI ZILIZOPO

NA

JINA

KATA

1

GEREZANI

GEREZANI

2

KIWALANI

KIWALANI

3

TABATA  A

TABATA 

4

TABATA  NBC

TABATA 

5

KINYEREZI

KINYEREZI

6

MONGO LA NDEGE

MONGO LA NDEGE

7

BONYOKWA

KINYEREZI

8

TABATA RELINI

TABATA 

9

VINGUNGUTI

VINGUNGUTI

10

BUYUNI

CHANIKA

11

KITUNDA

KITUNDA

12

KIPAWA

KIPAWA

13

KIVULE

KITUNDA

14

MVUTI

MVUTI

15

MVULENI

MSONGOLA

16

ZINGIZIWA

CHANIKA

17

MSONGOLA

MSONGOLA

18

YONGWE

CHANIKA

19

GULUKA KWALALA

GONGO LA MBOTO

20

SEGEREA

SEGEREA

21

GONGO LA MBOTO

GONGO LA MBOTO

22

MAJOHE

PUGU

23

Idc Clinic

Huduma zinazotolewa  katika vituo vya Zahanati hizi ni:-

· Matibabu ya magonjwa mbalimbali

· Huduma ya afya ya uzazi,ni pamoja na chanjo, makuzi , ujauzito, uzazi salama, uzazi wa mmpango

· Kufanya vipimo mbalimbali (maabara)

Idadi ya vituo vya tiba na wamiliki wake

Aina ya kituo

Mmiliki

Jumla

Serikali

Mashirika ya dini

Mashirika ya umma

Binafsi

1

Hospitali

2

3

0

4

9

2

Vituo vya Afya

2

8

1

11

22

3

Zahanati

24

10

9

110

153

4

Zahanati za majeshi/Polisi

9

0

0

0

9

5

Kliniki (maalum)

1

JUU