Elimu Sekondari

Elimu Sekondari

IDARA YA  ELIMU SEKONDARI.

Idara ya  Elimu Sekondari in jumla ya shule 97. Kati ya  hizo,  shule  49 za Serikali na shule 48 za binafsi/Mashirika ya dini. Shule za Serikali zina jumla ya wanafunzi 46,063 wakiwemo wavulana 22,388 na wasichana 22,675.  Shule za binafsi/Mashirika ya dini zina wanafunzi 13,571 Wakiwemo wasichana 6,644 na wavulana 6,927.Hivyo jumla ya wanafunzi wote ni 59,634 wakiwemo wavulana  29,315 na wasichana 30,319.

Halmashauri ina vyuo 03  vya Walimu vinavyotoa stashahada  na cheti. Kuna vituo 14 vinavyotoa  Elimu ya Sekondari kwa wanafunzi waliokosa Elimu hiyo kwa kupitia mfumo rasmi.

Halmashuri ina  shule mbili zinazochukua wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.  Shule hizo ni Jangwani na Pugu Sekondari.  Shule ya sekondari B.W.Mkapa inachukua  wanafunzi viziwi.

 Majukumu ya idara ya elimu sekondari.

Ø  Kusimamia utoaji wa elimu bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa

Ø  Kusimamia  na kufafanua sera na nyaraka mbalimbali za Elimu katika ngazi ya Halmashauri.

Ø  Kusimamia uendeshaji wa shule za sekondari katika halmashauri

Ø  Kusimamia  na kuratibu uendelezaji na ujenzi wa shule za Sekondari za Serikali.

Ø  Kusimamia mapato  na matumzi ya fedha katika shule za sekondari za Serikali

Ø  Usimamizi na uendeshaji wa  mitihani ya Mock na ya Taifa  ya kidato cha II,IV,VI na mitihani ya vyuo vya Ualimu.

Ø  Kushughulikia masilahi  ya Walimu na watumishi wasio Walimu waliopo katika shule za Sekondari kwenye Halmashauri.

Ø  Kuratibu uanzishaji wa shule za Sekondari

Ø  Kusimamia na kuendeleza michezo shuleni.

Ø  Kukusanya,kuchambua na kuunganisha Takwimu mbalimbali za shule za  Sekondari. 

JUU