Maji

Maji

 IDARA YA  MAJI.

Idara ya Maji  ipo kwa mujibu wa muundo wa Utumishi. Idara  ina vitengo vikuu vitatu.

Kitengo cha mipango na usanifu

Kitengo cha  ujenzi

Kitengo cha uendeshaji wa miradi ya maji na matengezo vinavyotambuliwa kisheria.

 Malengo/Majukumu ya Idara ya Maji

  Kuandaa bajeti ya kutekeleza miradi ya maji na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo

  Kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Manispaa wasiopata huduma  ya maji kutoka kwa mamlaka ya DAWASA na Kampuni ya DAWASCO.

Ø  Kutoa huduma ya uzoaji maji taka kwenye sehemu ambayo magari makubwa ya kuzoa maji taka hayafiki kwa kutumia pikipiki yenye miguu mitatu na pampu maalumu ya kuvuta maji taka.Kutoa mafunzo, kusimamia mchakato wa kuunda vyombo vya kusimamia na kuendesha miradi ya maji pamoja na kuvisajili, kwa

Ø  mujibu na taratibu wa  Sheria ya Maji ya 2009.

Ø  na kuendesha miradi ya maji kutunza fedha za matengezo na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za mfuko.

Ø  Japo kwa kiwango kidogo, kuweza kuchangia kukusanya mapato ya Halmashauri kupitia ukusanyaji wa fedha zinazotokana na upimaji wa maji katika maabara ya Idara ya Maji na ukataji wa vibali kwa wachimbaji wa visima wanaofanya kazi ndani ya Manispaa yetu.

Ø  Kupunguza na kuzuia  milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama

Ø  Kusimamia vyema miradi inayofanya kazi kwa kusisitiza vyombo vya kusimamia

Vitengo  vinaunda sehemu kumi na moja katika Idara. Idara ya Maji ina jukumu kubwa la kutoa huduma ya maji  kwa wakazi wa Manispaa ya Ilala. Pamoja na jukumu la kutoa huduma ya maji  Idara inahusika na kupanga na kusanifu miradi ya maji, kupitia usanifu wa miradi ya maji unaofanywa na wataalam wa nje, kusimamia ujenzi na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kukarabati miradi ya maji yenye hitilafu. Idara pia inahusika na kuunda na kusimamia vyombo vya watumiaji maji  

JUU