Mifugo na Uvivu

Mifugo na Uvivu

 MIFUGO NA UVUVI

Muundo wa Idara:

Idara ya Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili ambazo ni:

Ø  Mifugo na

Ø  Uvuvi

 Majukumu ya Idara:

Jukumu kuu la Idara ni pamoja na usimamizi wa shughuli zote zinazohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Serikali Kuu na Wadau mbalimbali katika sekta. Baadhi ya shughuli hizo ni pamoja na:-

Ø  Kusimamia shughuli za udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ya mifugo ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo.

Ø  Kusimamia ubora na usalama wa mazao yatokanayo na mifugo na uvuvi

Ø  Kuratibu na kusimamia sheria mbali mbali za mifugo na uvuvi

Ø  Kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazohusiana na maandalizi na ushiriki wa mikutano ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na sherehe mbalimbali za mifugo na uvuvi kama za wakulima Nanenane, zinazofanyika kila mwaka kwenye viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere, mkoani Morogoro na siku ya chakula duniani.

Ø  Kusimamia na kuratibu shughuli zinazofanyika katika umiliki wa Manispaa ya Ilala kama majengo ya Manispaa yaliyopo chini ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kama vile; machinjio ya Vingunguti, Banda la Maonesho ya Kilimo, Nanenane mkoani Morogoro na banda la kuendeleza ufugaji kuku wa kienyeji, Mvuti.

Ø  Kusimamia mapato yatokanayo na ushuru wa Mifugo, samaki na mazao yake.

Ø  Kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiutawala na utumishi wa wataalam wa mifugo na uvuvi.

Ø  Kuratibu na Kusimamia ukusanyaji wa ushuru, tozo, ada, na leseni zinazohusiana na sekta ya mifugo na uvuvi. 

JUU