Maendeleao ya Jamii na Ustawi wa Jamii

Maendeleao ya Jamii na Ustawi wa Jamii

MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII

Idara ya Maendeleo Ustawi wa Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara zilizopo katika Halmashauri za Manispaa, Mji na Wilaya kwa mujibu wa maelekekezo ndani ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Idara hii ina jumla ya vitengo vikuu vitatu ambavyo ni:-

Ø  Maendeleo ya Jamii

Ø  Ustawi wa Jamii na

Ø  Vijana

Ø  Majukumu ya Idara

Ø  Idara ina jukumu la kuhudumia jamii katika Nyanja mbalimbali kwa kuzingatia umri, rika, na jinsi bila ubaguzi wa rangi, utaifa, kabila mila na desturi. Dhumuni la Idara ni kuleta Ustawi na Maendeleo ya jamii kuanzia mtu mmoja mmoja, vikundi na jamii kwa ujumla.

 Majukumu ya sehemu ya maendeleo ya jamii:

Ø  Madhumuni ya Sehemu hii ni kuleta mabadiliko katika Jamii kwa kushirikisha wananchi, Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika nyanja za kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni.

 

Majukumu na kazi kwa kila kitengo:

Utafiti na mipango

Ø  Kukusanya, kuchambua na kuhakiki taarifa mbalimbali za kijamii kutoka mitaa na Kata na kupendekeza kushauri miradi mbalimbali kwa ajili ya wananchi,

Ø  Kuratibu shughuli za sehemu ya Maendeleo ya Jamii na kuziandikia mipango ya utekelezaji,

Ø  Kubuni mbinu mbalimbali za kushirikisha wananchi katika mipango ya maendeleo,

Ø  Kufanya utafiti wa awali na utafiti wa kina juu ya miradi inayopendekezwa na wananchi na kutoa taarifa,

Ø  Kutoa huduma kwa wananchi kupitia jumuiya , vikundi au binafsi vya uzalishaji na usimamizi wa miradi ya kiuchumi na kijamii

Ø  Kuandaa mafunzo ya watumishi wa sehemu ya maendeleo ya Jamii,

Ø  Kuandaa mafunzo kwa viongozi wa wananchi na makundi mbalimbali katika Jamii

Ø  Utunzaji wa Takwimu muhimu zinazohusu watu na mazingira yao mfano; idadi ya watu huduma za kijamii na kiuchumi zilizopo.

   Jinsia na maendeleo ya watoto

Ø  Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya wanawake na watoto,

Ø  Kuingiza suala la jinsia katika mipango yote ya maendeleo ya jamii,

Ø  Kutoa mafunzo kwa wanawake kupitia vikundi vya uzalishaji mali na utoaji huduma juu ya wajibu na nafasi ya wanawake katika jamii,

Ø  Kutafuta kusimamia na kuratibu mikopo na misaada inayolenga kuleta kuleta ukombozi kwa wanawake,

Ø  Kusimamia kutekeleza sera za maendeleo ya wanawake na watoto katika kupiga vita umasikini na kuondoa suala la ajira kwa watoto.

 Usajili wa NGOS

Ø  Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs kuanzia ngazi ya mtaa, kata hadi Manispaa,

Ø  Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji udhibiti na ubora wa takwimu zinazohusu mashirika yasiyo ya Kiserikali,

Ø  Kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya Serikali kwa kuzingatia mipangokazi iliyoainishwa baada ya kupata usajili,

Ø  Kuhakiki na kuratibu shughuli za jumuiya za watumia maji ngazi ya mtaa kata hadi Manispaa.

 Kudhibiti UKIMWI

Ø  Kuratibu na kusimamia shughuli za mwitikio dhidi ya VVU/UKIMWI katika Halmashauri,

Ø  Kushirikiana na wadau (asasi na watu wanaoishi na vvu) kutengeneza mpango wa Halmashauri wa mwitikio wa VVU na UKIMWI,

Ø  Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya VVU kwa kutumia njia mbalimbali kama sanaa shirikishi, sinema, semina, warsha nk,

Ø  Kuratibu ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za huduma za UKIMWI kupitia mfumo wa TOMSHA

Ø  Kuimarisha shughuli a kiuchumi na kuongeza kipato kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI,

Ø  Kutoa misaada kwa makundi, familia na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

   Sekta isiyo Rasmi

Ø  Kuainisha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo kwa kushirikiana na sekta zingine

Ø  Kuandaa, kuratibu, kuwatambua na kuwaorodhesha wafanyabiashara walioko kwenye sekta isiyorasmi

Ø  Kuhamasisha uundaji wa vikundi vya wajasiliamali wa sekta isiyo rasmi

Ø  Kuandaa na kuendesha mafunzo ya wajasiliamali kuhusu uwekezaji, kudhibiti UKIMWI, jinsia na sheria mbalimbali za Halmashauri

Ø  Kuwaunganisha wajasiliamali wa sekta isiyo rasmi na wadau wengine ili waweze kutumia fursa zilizopo.

   Kazi na Majukumu ya Sehemu ya Ustawi wa Jamii

Sehemu ya Ustawi wa Jamii ina wajibu wa kusimamia utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kwa wananchi mbalimbali wenye matatizo ya kijamii yanayohitaji ufumbuzi wa Kiustawi.  Huduma hizo zinatolewa kwa wananchi wa jinsi zote wakiwemo wazee, watu wenye ulemavu, watoto, wajane na wagane bila ubaguzi wa rangi na kabila.

MAJUKUMU NA KAZI KWA KILA KITENGO:

   Huduma za ustawi wa familia na watoto

  Kuratibu na kusimamia huduma zote zinazolenga kuimarisha ndoa na familia kwa ustawi wa wanandoa na watoto mfano; kuratibu mashauri ya ndoa, mashauri ya matunzo ya watoto ndani na nje ya ndoa, kuasili,nk.

  Kuratibu usajili na ukaguzi wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009

  Kuratibu usajili na ukaguzi wa makao ya kulelea watoto walio katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009

  Kuratibu huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa mpangokazi wa kitaifa wa kuhudumia watoto walio katika mzingira hatarishi

  Kuratibu na kusimamia ulinzi na usalama kwa watoto kuanzia ngazi ya mtaa, kata na Halmashauri kupitia timu za ulinzi na usalama wa mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 na kanuni za ulinzi na usalama wa mtoto.

   Marekebisho ya tabia na haki za watoto kisheria

  Kuratibu na kusimamia mabadiliko ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria

  Kuratibu na kusimamia haki za watoto walio katika mkinzano na sheria mbalimbali za nchi

  Kuratibu na kusimamia kesi/mashauri yote ya watoto waliokatika mkinzano na sheria mahakamani

  Kuratibu na kusimamia kesi/mashauri ya watoto waliguswa na sheria mahakamani.

Huduma za ustawi hospitali na vituo vya afya

  Kuratibu na kusimamia huduma zote za kiustawi Hospitalini na katika viyuo vya Afya

  Kuratibu na kusimamia Msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wasio na uwezo wa kugharamia matibabu

  Kuratibu na kusimamia mfumo wa Tiba kwa Kadi (TIKA)

  Kuratibu na kusimamia dirisha la wazee hospitali na viyuo vya afya.

Utengamao wa Wazee na Watu wenye Ulemavu

  Kuratibu na kusimamia utengamao kwa wazee na watu wenye ulemavu

  Kuratibu na kusimamia vikundi, SACOS kwa watu wenye ulemavu

  Kuratibu ukusanyaji wa takwimu za wazee na watu wenye ulemavu katika Halmashauri

  Kuratibu mikopo midogomidogo kwa watu wenye ulemavu na wzazee.

 Sehemu ya Vijana

Sehemu ya vijana inajukumu la kutoa huduma kwa vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala huduma hizo ni pamoja na kuunda vikundi vya ujasiriamali, utoaji wa elimu ya uzazi wa Afya, stadi za kazi, Ujasiriamali, madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya na kundi la vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi kama vile dada poa na kaka poa. 

JUU