Ujenzi na Zimamoto

Ujenzi na Zimamoto

IDARA YA UJENZI NA ZIMAMOTO

Idara ya Ujenzi ina jukumu la kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi zinazohusika na miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua, usimamizi wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya serikali, matengenezo ya magari na mitambo ya Halmashauri, na ukaguzi wa majengo  yanayojengwa katika Manispaa ya Ilala, kusimamia mchakato wa vibali vya ujenzi, usalama wa barabara na udhibiti wa magari, uwekaji wa mabango na uzio wa kuzingira na uwekaji wa umeme kwenye majengo ya Serikali. Pia Idara inaratibu mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Mentropolitan Development Project- DMDP).

Mgawanyo wa majukumu

Katika kutekeleza majukumu yake Idara imegawanywa katika sehemu (sections) kuu tisa (9) kama ifuatavyo:

Ø  Sehemu ya Barabara;

Ø  Sehemu ya Ukaguzi wa Majengo;

Ø  Sehemu ya Vibali vya Ujenzi;

Ø  Sehemu ya Mifereji ya Maji ya Mvua;

Ø  Sehemu ya Usalama na Udhibiti wa Magari;

Ø  Sehemu ya Mabango na Uzio;

Ø  Sehemu ya Umeme;

Ø  Sehemu ya Karakana na Mitambo;

Ø  Sehemu ya Miradi ya Majengo ya Serikali.

Sehemu ya ukaguzi wa majengo

Sehemu ya Ukaguzi wa Majengo hufanya kazi za ukaguzi wa majengo yanayojengwa maeneo mbalimabali ya Manispaa ya Ilala kwa kusimamia Sheria na taratibu za ujenzi.

Zifuatayo ni shughuli zinazosimamiwa na kitengo hiki kuhakikisha kwamba:-

Ø  Ujenzi na Ukarabati unaofanyika unakuwa na kibali cha ujenzi kutoka Manispaa ya Ilala,

Ø  Michoro ya ubunifu wa ujenzi huo  imeidhinishwa na Manispaa ya Ilala,

Ø  Iwapo kuna mabadiliko katika michoro ya ujenzi yawe yamepata idhini ya Halmashauri,

Ø  Ujenzi umeanza ndani ya muda wa miezi sita tangu kutolewa kwa kibali cha ujenzi,

Ø  Jengo linatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa,

Ø  Eneo la mradi limezungushiwa uzio na kuwekewa vizuia kwa ajili ya usalama wa watu na mali zao.

Ø  Upimaji wa vifaa vya ujenzi unafanywa na kumbukumbu zinakuwepo na kutunzwa katika eneo la mradi,

Ø  Kuna bango kwenye eneo la mradi na likionesha wanaohusika kwenye ujenzi na uwepo wa Wataalamu wa ujenzi huo na

Ø  Majengo yanapatiwa hati za kuhamia.

Sehemu ya vibali vya ujenzi

 Majukumu ya Sehemu

Majukumu ya sehemu ya Vibali vya Ujenzi ni pamoja na;

Ø  Kupokea maombi mbalimbali ya vibali vya ujenzi,

Ø  Kuweka  kumbukumbu za maombi yanayopokelewa na kuyapa namba za Usajili,

Ø  Kuweka ada ya uchunguzi,

Ø  Kukagua viwanja vinavyokusudiwa kuendelezwa.

Ø  Kukagua michoro ya majengo kuhusu masuala yanayohusu usanifu wa majengo.

Ø  Kuratibu mchakato wa uchunguzi  unaofanywa na wataalam wa Idara mbalimbali,

Ø  Kuandaa maombi yanayokidhi masharti na kuyawasilisha kwenye Kikao cha Kamati Ndogo ya Vibali vya Ujenzi,

Ø  Kuandaa vibali vya ujenzi na kuwasilisha kwa waweka saini.

Ø  Kuandaa Hati za Kuhamia majengo mapya yaliyokamilikana kuwasilisha kwa waweka saini.

Sehemu ya mifereji ya maji ya mvua

 Majukumu

Sehemu ya mifereji  ya maji ya mvua  ina jukumu la kuzuia mafuriko yasiyo ya lazima yasitokee barabarani na kwenye makazi ya watu. Zifuatazo ni kazi za sehemu ya mifereji:

Ø Kusimamia matengenezo na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua

Ø Kusimamia ukarabati wa wavyoo vya shule na vyoo vya umma.

Ø  Kufanya usanifu wa mifereji na makisio ya ujenzi huo.

Ø  Kuandaa mpango wa manunuzi (procurement planing).

Ø  Kuandaa nyaraka za zabuni na rasimu ya tangazo la zabuni kwa kazi zote za mifereji ya maji ya mvua kwa kushirikiana na Afisa Manunuzi wa Manispaa.

Ø  kufanya tathmini ya hali ya mifereji ya maji ya mvua na kutoa ushauri wa kitaalam.

Kuandaa makisio ya bajeti ya mifereji ya maji ya mvua

Sehemu ya usalama barabarani na mabango

Kitengo cha Usalama Barabarani na Mabango kinahusika na Usalama wa barabara na bakaa zake pamoja na utoaji wa vibali vya mabango ya matangazo.

Usafiri katika Manispaa ya Ilala kama ilivyo kwenye maeneo mengine mijini ni muhimu kwa maendeleo ya wakazi wake. Kufuatana na eneo la Manispaa kijiografia kuwa katikati ya Jiji ukilinganisha na Manispaa nyingine kama vile Temeke na Kinondoni na pia kuwa na eneo kubwa la biashara pamoja na ofisi nyingi na hivyo kuwavutia watu wengi, suala la usafiri na usafirishaji linahitaji kuangaliwa kwa umuhimu wa pekee. Sehemu ya Usalama na udhibiti wa magari pamoja na mabango katika idara ya Ujenzi ndiyo inajukumu la kuhakikisha usalama barabarani na udhibiti wa magari mjini na usimamizi wa uwekaji wa mabango na uzio. Baadhi ya shughuli za sehemu hii ni pamoja na:

  Kusimamia uwekaji na matengenezo ya alama za barabarani;

  Kusimamia Matengenezo na kudhibiti usalama wa njia za waenda kwa miguu,

  Ukaguzi wa vituo vya Teksi,

  Kutoa vibali maalumu kwa magari yenye uzito wa zaidi ya tani tatu na nusu hadi kumi kwa shughuli za ujenzi katikati ya jiji,

  Kudhibiti magari makubwa (Makontena) yanayofanya shughuli katikati ya jiji na kuyatoza faini,

  Kufanya tathimini na usimamizi wa ujenzi wa maegesho na vituo vya daladala,

  Kusimamia uwekaji wa majenereta katika maeneo ya mjini,

  Kusimamia uwekaji wa Mabango pamoja na uzio wa kuzingira maeneo ya majenzi.

  Kudhibiti matumizi mabaya ya barabara.

 Sehemu ya Umeme

Kitengo cha umeme Manispaa ya Ilala kina jukumu la kusimamia kazi zote zinazohusiana na umeme ndani ya Manispaa ya Ilala. Kazi hizo ni kama ifuatavyo:-

Ø  Kusimamia mifumo yote ya umeme katika majengo yote yalio chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Ø  Kukagua mifumo yote ya umeme kwenye majengo mapya ya Manispaa.

Ø  Kubuni “designing” mifumo mipya ya umeme kwa ajili ya majengo ya Manispaa.

Ø  Kurekebisha hitilafu zote za umeme zinazojitokeza kwenye mifumo ya umeme iliyopo kwenye majengo na ofisi za Manispaa.

Ø  Kutoa ushauri unaohusiana na kazi za umeme katika Manispaa.

Ø  Kubuni, kuandaa makisio ya pampu za maji pamoja na ufungaji wa pampu hizo katika visima vya Manispaa

Ø  Kufanya ukaguzi wa mifumo ya umeme kwenye majengo na taa za 

mitaani (street light).

Ø  Kubuni na kauandaa makisio kwa ajili ya uwekaji mfumo wa umeme

jua (solar power) kwa ajili ya majengo ya halmashauri yalipo pembezoni

ambako hakuna umeme wa Tanesco.

Sehemu ya Majengo

Majukumu

Majukumu yao ni pamoja na;

Ø Kufuatilia utendaji kazi wa wakandarasi wa ujenzi wa majengo kuhusu viwango vya utendaji kazi vya wakandarasi hao, ubora wa kazi na gharama za utekelezaji wa kazi hizo.

Ø Kuandaa michoro na maekekezo (specifications) na kufanya usanifu  (designs) wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo katika Halmashauri ya Manipaa ya Ilala.

Ø Kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya majengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ili kujiridhisha na ubora wa kazi, muda wa utekelezaji na  viwango vilivyowekwa vya utekelezaji.

Ø Kutayarisha taarifa za maendeleo ya miradi na shughuli za ujenzi wa majengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za mwezi, robo mwaka, nusu mwaka, mwaka mzima na muda mwingine wowote kadri itakavyotakiwa.

Ø Kukusanya Takwimu za shughuli mbalimbali za majengo na kutunza takwimu hizo katika mtindo na taratibu zinazokubalika ili kuruhusu upatikanaji rahisi wa Takwimu hizo pale zinapohitajika kwa matumizi mbalimbali.

Ø Kuhudhuria vikao vyote vya Halmashauri na Serikali kuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kulingana na utaratibu uliowekwa na kutekeleza maazimio mbalimbali ya vikao hivyo yanayohusu Idara ya Ujenzi na Maji.

Ø Kutoa ushauri kwa Mkuu wa Idara kuhusu masuala yote ya kitaalam yanayohusiana na shughuli za ujenzi wa majengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Ø Kushirikiana na Idara  na Vitengo vingine vya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na nje ya Halmashauri ya Manispaa ya Iala ili kuhakikisha kwamba majukumu ya Kitengo cha Majengo yanatekelezwa  ipasavyo.

Ø Kupitia, kupendekeza na kushauri mabadiliko yoyote ya kisheria ili kukidhi matakwa ya utendaji kazi katika kitengo cha Majengo.

Ø Kukusanya na kuweka kumbukumbu (Contract documents) kwa kila mradi ulioko kwenye wa ngazi ya Halmashauri, kata na shule na miradi yote inayofadhiliwa na wahisani. 

JUU