Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu

Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu

IDARA YA  MAZINGIRA NA UDHIBITI TAKA NGUMU

Idara ya Uhifadhi wa Mazingira na udhibiti taka ngumu inashughlika na majukumu mbalimbali yanayohusu usafi wa  Manispaa ikiwa ni pamoja na kuandaa kusimamia mipango/mifumo mbalimbali inayohusu usafi na uhifadhi wa mazingira pamoja na uboreshaji wa mandhari kwa ujumla.

  Majukumua ya Idara

Ø  Kupanga na kusimamia huduma ya Uondoshaji wa taka

Ø  Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya huduma mbalimbali za usafishaji wa manispaa.

Ø  Kutoa huduma ya uondoshaji wa maji yaliyotuama na maji taka kwenye mifereji iliyoziba,  toka maeneo huduma makazi na majengo ya Halmashauri kama vile Zahanati , machinjio, masoko na shule n.k

Ø  Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Wakandarasi na vikundi vya kijamii vinavyotoa huduma za usafishaji.

Ø  Kuratibu huduma za uondoshaji taka hatarishi, kama vile taka za Hospitali na viwandani.

Ø  Kuandaa mipango ya kuboresha mazingira (Environmental Plan) hii ni kwa mujibu wa sehemu ya nne (part IV) ya sheria ya mazingira.

Ø  Kulinda, kuhifadhi na kuboresha Mazingira (Environmental Management and Beautification) Kwa mujibu wa sehemu ya tano (part v) ya sheria ya mazingira.

Ø  Kupitia (review) tathmini ya athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment) hii ni kwa mujibu wa sehemu sita (part VI) ya sheria ya mazingira.

Ø  Kuzuia uchafuzi wa mazingira (Pollution prevention control) Kwa mujibu wa sehemu ya nane (part viii) ya sheria ya mazingira.

Ø  Kusimamia viwango vya ubora vya mazingira (Environmental quality standards) Kwa kushirikiana na NEMC na taasisi /sekta zingine hii ni kwa mujibu wa sehemu ya kumi (part x) ya sheria ya mazingira.

VITENGO VILIVYOPO CHINI YA MKURUGENZI.

KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni miongoni mwa vitengo sita (6) vilivyo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi. Kitengo hiki kimeundwa kwa Kifungu Na. 48 cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 Halmashauri itaajiri Mkaguzi wa Ndani ambaye atafanya kazi za ukaguzi kwa karibu na Wakuu wa Idara lakini atatoa taarifa moja kwa moja kwa Mkurugenzi.

· Sheria hiyo inampa uhuru/mamlaka Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri kuweza kufanya kazi za ukaguzi/uhakiki wa mifumo dhibiti ya ndani na kupima viwango vya ufanisi na utendaji wake wa kazi.

MAANA YA UKAGUZI WA NDANI

Ukaguzi wa Ndani ni shughuli huru ya ukaguzi inayofanyika ili kuhakikisha kama malengo yatafikiwa, pia kutoa ushauri utakaosaidia kutoa matokeo mazuri ya kazi mbalimbali za Halmashauri.  Ukaguzi husaidia Halmashauri kukamilisha malengo yake kwa kujihakiki na kupata ufanisi kwa kudhibiti vihatarishi, mifumo na michakato ya ndani.

MAJUKUMU MAKUU YA UKAGUZI WA NDANI

Kwa ujumla majukumu makuu ya Ukaguzi wa Ndani ni kusaidia Menejimenti ya Halmashauri katika kufanya uhakiki huru utakaotoa picha ya kufikiwa kwa malengo na kushauri juu ya ufanisi wa mifumo dhibiti ya ndani ya Halmashauri.

MAELEZO ZAIDI

Ni muhimu kuwa huru kutoka kwa menejimenti (lengo ni kuwa huru katika kutoa ushauri na maamuzi sahihi)  Ukaguzi wa Ndani utambulike kama chombo cha Menejimenti.  Hivyo Menejimenti inapaswa kutoa ushirikiano ambao utawezesha Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kufanya kazi kwa ufanisi na Halmashauri kuweza kufikia malengo.

MAJUKUMU MENGINE

Ø  HUDUMA ZA KUTOA UHAKIKISHO

Kuhakiki kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa

  Mchakato wa utawala bora.

Mchakato wa vihatarishi.

(c)  Mifumo dhibiti ya ndani.

· Kuhakiki michakato na kazi maalumu

Inaelezea mambo muhimu na baadhi ya aina za ukaguzi ambao hufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri /Serikali za Mitaa.

  Ukaguzi wa rasilimali fedha.

Ukaguzi wa miradi/thamani ya fedha.

  Ukaguzi wa rasilimali watu.

Ukaguzi wa manunuzi ya umma.

  Ukaguzi wa mifumo/mawasiliano.

Kufanya uchunguzi.

Ø  HUDUMA ZA USHAURI

Mkaguzi wa Ndani kutoa ushauri unaohusu shughuli, hali halisi na mipaka ya ukaguzi iliyokubaliwa na Halmashauri ambao unalenga kuongeza ufanisi katika Utawala bora, udhibiti wa vihatarishi, na mifumo dhibiti ya ndani ya Halmashauri. 

JUU