TANGAZO LA KUENDELEZA MAENEO YA WAZI KWA UBIA KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

1.0 Utangulizi

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inakusudia kuendeleza maeneo 20 ya wazi kwa ubia, na inakaribisha Wadau wa utunzaji wa Mazingira ili kuingia mkataba wa kuendeleza maeneo hayo. Maeneo yanayokusudiwa kwa kuanzia yanajumuisha Bustani za Mapumziko, Maeneo ya Wazi, Mizunguko ya barabara na Barabara kuu sehemu za katikati na pembeni.

2.0 Orodha ya Maeneo

Mchanganuo wa maeneo yanayokusudiwa kuendeshwa kwa ubia ni kama ifuatavyo:-

S/N

ENEO

MAHALI LILIPO

1.

Bustani za Mapumziko

Umoja wa Vijana Eneo la Wazi (Barabara ya Morogoro mkabala na Jengo la Vijana.

Palm Beach (Makabala na Palm Beach Hotel)

  Karimjee Botanical Garden

2.

Maeneo ya Wazi

Baclays (Mkabala na Hotel ya Royal Palm)

Stetesheni

  Viwanja vya Mnazi Mmoja No. 1 (Mashujaa)

  Viwanja vya Mnazi Mmoja No. 2 (Ofisi ya Kata Mchafukoge)

Viwanja vya Mnazi Mmoja No.3 (Viwanja vya Michezo)

  Cocabs (Eneo la wazi – Makutano ya barabara ya Lumumba na Nyerere)

Mahakama ya Kariakoo (Eneo la wazi-Makutano ya barabara ya Lumumba na Morogoro)

  Samora Mkabala na Benki ya NBC (Barabara ya Samora/ India)

   Mpilipili mkabala na Barabara ya Lithuri

3.

Mizunguko ya Barabara

Mzunguko wa Clock tower

Mzunguko wa Askari Monument na Eneo la wazi la Askari Monument (Balcon)

 

4.

Barabara

Barabara ya Nyerere

Barabara ya Kawawa

  Barabara ya Lumumba

  Barabara ya Bibi Titi

Barabara ya Uhuru

  Barabara ya Sokoine

Barabara ya Luthuli

3.0 Mashartiya Muombaji

Halmashauri itachangia eneo la ardhi na itaingia Mkatataba na Muombaji kwa masharti yafuatayo:-

  1. Mwombaji atakuwa ni mpangaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
  2. Mwombaji awasilishe maombi ya eneo analotaka kuendeleza na rasimu ya Mkataba wa uendelezaji kwa Mkurugenzi ambao utarekebishwa/ utahakikiwa kabla ya kusainiwa.
  3. Mwombaji abainishe na kuthibitisha uwezo wake kifedha, nyenzo, wataalamu, uzoefu na uhusiano wa shughuli zake kwa sasa na jinsi zitakavyochangia kuboresha eneo husika
  4. Mwombaji hataruhusiwa kujenga jengo la kudumu au kufanya biashara kinyume na matumizi yaliyokusudiwa kwenye eneo analoomba.
  5. Mwombaji aonyeshe manufaa atakayopata katika usimamizi na uendelezaji wa eneo hilo.
  6. Baada ya makubaliano na kuingia mkataba, Halmashauri haitagharamia maeneo hayo katika kipindi cha mkataba.

Maombi yote yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kabla au ifikapo tarehe 14.09.2015.

Isaya M. Mngurumi

MKURUGENZI WA MANISPAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA