TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA MSONGOLA

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA  KWA  KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA TANZANIA REMIX CENTRE LIMITED INAKUSUDIA KUUZA VIWANJA 1200 VILIVYOPIMWA KWA MATUMIZI MBALIMBALI. VIWANJA HIVYO VIPO KATA YA MSONGOLA KANDOKANDO YA BARABARA YA LAMI ITOKAYO CHANIKA KUELEKEA MBAGALA NA PIA VIPO KARIBU NA MIUNDOMBINU MUHIMU.

FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA KATIKA OFISI ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA ZILIZOPO ENEO LA ARNATOUGLOU-MNAZI MMOJA KWA GHARAMA YA TSHS. 30,000/= KILA MOJA.

FOMU ZITAANZA KUUZWA TAREHE 01/09/2015 HADI TAREHE 14/09/2015 MUDA NI KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI HADI SAA 9:30 ALASIRI.

BEI ZA VIWANJA KWA UJAZO WA JUU, KATI NA CHINI KWA MITA MOJA YA MRABA NI KAMA IFUATAVYO;

 

1. Viwanja vya Makazi Tshs. 10,000/=

2. Viwanja vya Biashara Tshs. 12,000/=

3. Biashara Pekee Tshs. 15,000/=

4. Kuabudia Tshs. 8000/=

WATU WOTE MNAKARIBISHWA

Limetolewa na,

 

 

Isaya M. Mngurumi

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA