Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ni mojawapo kati ya Halmashauri zilizopo katika jiji la Dar es Salaam. Halmashauri hii inatoa huduma mbalimbali kwa wakazi wake zikiwemo Elimu, Afya, Usafi wa jiji, Biashara, Barabara, Sheria na Utawala Bora, masuala ya Ardhi na Mipango miji, ukusanyaji wa mapato, huduma za Mifugo na kilimo, Ushirika na Maendeleo ya Jamii, huduma za maji (Visima) na nyinginezo. Pamoja na utoaji wa huduma hizi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inayo Dira na Jukumu kuu: • Jamii yenye maisha bora, inayopata huduma bora, inayopata huduma za msingi na kuondoa umaskini kwa kiasi kikubwa ifikapo mwaka 2015. • Kujenga uwezo wa Halmashauri wa kutoa huduma za Kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake na hivyo kuondoa umaskini na kuinua hali zao za maisha.